
Habari Mpya toka kenya zinaarifu kuwa,Watu 500 wameokolewa huku 147 wakiuawa wakiwemo wapiganaji wote wa kundi la Al shabaab wanne waliokuwa
wamevamia na 79 kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa kituo cha Televisheni cha K24 cha nchini Kenya, majeshi ya KDF Yakisaidiana na Polisi yamefanikwa kuwaua magaidi wote na kuchukua udhitibi wa chuo hicho.
Mapigano Hayo Yamechukua Masaa 14 Kukamilika.

