Askari wa FFU wakiwa katika msako wa kuwasaka waliohusika na vurugu hizo eneo la Ipogolo mjini Iringa
Polisi wakie;ekea emeo la tukio
Baadhi ya watuhumiwa wa vurugu hizo wakipakiwa katika gari la FFU
Wananchi
wakiwa katika vurugu hizo huku baadhi yao wakishuhudia Mpita njia
eneo la Ipogolo akipiga picha kwa simu moto uliokuwa ukiwaka
barabarani
***********
Na MatukiodaimaBLOG
VURUGU
kubwa zimetokea leo katika eneo la Ipogolo mjini Iringa na
kupelekea askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) kutumia
mabomu ya machozi kuthibiti vurugu baada ya mtoto wa miaka kata 6
kugongwa na gari wakati akifanya biashara ya kuuza mbogo mboga .
Wananchi
wanaosadikika kuwa na hasira kali walianza kuwashambulia askari
polisi waliofika kuchukua mwili huo kwa mawe kwa madai ya kuchelewa
kufika eneo la tukio.
Wakizungumzia
tukio hilo kwa mwandishi wa habari hizi baadhi ya wananchi
walisema kuwa mtoto huyo aligongwa majira ya saa 7 mchana na zaidi
ya saa moja baada ya kutoa taarifa polisi ndipo walipofika eneo
la tukio jambo lililowakwaza wananchi hao .
Walisema
kuwa mbali ya polisi hao kufika pia tayari baadhi ya askari
waliopo eneo hilo la stendi kuu ya Ipogolo kwa kushirikiana na
wananchi walifanikiwa kulikamata gari ambalo lilisababisha ajali
hiyo .
Alisema
Neema Sanga kuwa wakati tukio la kugongwa mtoto huyo likitokea
alikuwa jirani na eneo hilo katika msiba na kuwa wakati akiwa
ameingia ndani ya nyumba hiyo yenye msiba kusaidia kugawa chakula
ghafla alipata taarifa kuwa wananchi wameanza vurugu kwa kuchoma
moto matali katika barabara hiyo kuu ya Iringa- Kilolo.
Hata
hivyo alisema kuwa tukio hilo lilichukua zaidi ya dakika 45
polisi hao wa FFU kufika na kuanza kutuliza vurugu hizo kwa kupiga
mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi zaidi ya 500 waliokuwa
wamekusanyika eneo hilo kuzuia magari kuendelea kupita katika
barabara hiyo huku baadhi yao wakitaka kufunga barabara kuu ya
Mbeya - Iringa ambayo haihusiki ka bisa na eneo lililotokea tukio
hilo.
"
Ni kweli mtoto kagongwa na gari na kufa tukio ambalo ni kusikitisha
sana na polisi baada ya kupigiwa simu wamefika eneo la tukio na
kuchukua maiti ya mtoto huyo lakini tunajiuliza kwanini vijana hao
kuanza kuwapiga mawe polisi na kufanya vurugu wakati gari
lililogonga mtoto huyo likiwa limekamatwa .." alihoji Bi sanga
Kuwa
kwa upande wake hakuona sababu za polisi kupigwa wala wananchi
hao kuchoma moto barabara wakati ajali hiyo kama ajali nyingine na
tayari gari lililosababisha ajali likiwa limekamatwa .
Bi
Sanga alisema wakati mwingine polisi wanalalamikiwa kuwa
wanatumia nguvu zaidi ila kwa tukio hilo lawama zake anazipeleka
kwa wananchi wenzake ambao walionyesha kufanya vurugu kwa kuchomo moto
barabara hiyo ya lami na kupiga polisi huku wakitambua wazi
polisi si waliosababisha ajali hiyo.
Huku
kwa upande wake mmoja John Kalinga akiomba serikali kupitia
wizara ya miundo mbinu kuangalia uwezekano wa kuweka matuta katika
eneo hilo kwa madai kuwa hii ni ajali ya pili kutokea na kusababisha
vifo toka eneo hilo lilipowekwa lami .
Mwandishi
wa habari hizi alishuhudia baadhi ya vijana wakikimbilia kujificha
katika nyumba moja iliyopo eneo hilo ambayo ilikuwa na msiba huku
baadhi yao wakijifungia katika maduka na bar zilizopo eneo hilo
kabla ya polisi kuwafuata na kuwakamata huko walikojificha na
kuwaacha wale waliokimbilia msibani .
Kamanda
wa polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi hakuweza kupatikana
kuzungumzia tukio hilo huku idadi ya vijana waliokamatwa kwa tuhuma
za kuhusika katika vurugu hizo zaidi ya 20 walionekana wakipagiwa
katika magari ya polisi.