Wema
Sepetu ni mwigizaji staa wa Tanzania hakuna asiejua, Wema Sepetu ni
Miss Tanzania 2006 na ni miongoni mwa mastaa wenye ushawishi mkubwa
kwenye mitandao ya kijamii,
hakuna asiejua…… ila tatizo linalomsumbua
kwa sasa inawezekana kuna wengi wasiolijua.
Amekua akisumbuliwa na tatizo la kutoweza
kushika ujauzito ambapo baada ya ukimya mwingi, Wema ameamua kuongea
yafuatayo kwa wote wanaombeza kutokana na tatizo lenyewe.
Amesema >>> ‘Ningekuwa
na uwezo wa kuzaa ningekuwa nimezaa muda mrefu sana… But sina… Na
siwezi kumkufuru mwenyezi mungu…. Au mngependa niwe nawaambia jinsi
ninavyo hangaika usiku na mchana kupata mtoto wangu mwenyewe… Is dat wat
u want…? kila ntakachofanya kwa ajili ya tumbo langu basi nitangaze… Au
mnadhani siumii mnavyosema kuhusu maswala ya mtoto‘
Sentensi ya pili >>> ‘Kumbukeni
na mimi pia ni binaadam… nina moyo kama nyie… au mnadhani napenda kuona
wenzangu wana watoto au wana ujauzito alafu mimi sina hata wa
kusingiziwa… mnaona nafurahia sio…. hivi mna nini jamani… yaani mtu
unaweza weka post kwa nia nzuri then people jus come from nowea wanaanza
kukuandikia maneno ya kukuumiza kabisa nafsi hadi mtu unakaa unajiuliza
umemkosea nini mwenyezi Mungu‘
‘Kwani kuna
niliemkosea yoyote mpaka muanze tu kunikashif na kunitolea maneno mazito
namna hio… Kisa mtoto… mnadhani naipenda hii hali… hata mimi natamani
kuitwa mama na hakuna kinachoniuma kama hicho…. So mnadhani sijui kama
umri unaenda na maisha yenyewe sikuhizi mafupi anytime we die…
Mnafikiria nisingependa kuacha hata ka copy kangu siku ndo Mungu anasema
ananichukua’
‘Hata
mimi natamani ningekuwa napiga picha niko na mwanangu… I want dat with
all my life but I cant…. Sitokaa nimkufuru Mungu wangu hata siku moja
maana sijui ni kitu gani kaniandikia… But just dont rub it in… It hurts…
And im jus a human being like each and everyone of u….