Wachezaji
wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania wakiongozwa na Patrick
Kluivert (aliebeba mtoto) wakiingia uwanjani tayari kwa kukipiga na timu
ya Tanzania Veterans katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja
wa Taifa, Jijini Dar es salaam. hadi mwisho wa mchezo, Barcelona ya
Hispania ilishinda bao 2-1.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
Mchezaji
wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania, Patrick Kluivert akifurahia
jambo na Mtoto mwenye Ualbino kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa
kirafiki dhidi ya Tanzania Veterans uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa,
Jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo, pia kulikuwa na ujumbe wa Harakati ya Imtosha ikiwa ni kupiga vita mauaji ya watu wenye Ualbino nchini.