MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), wamesema hawajapata taarifa rasmi juu ya mgomo wa wamiliki wa mabasi ya mikoani.
Akizungumza
na MPEKUZI kwa njia ya simu jana, Ofisa Habari wa Sumatra, Daud
Mziray, alisema hakuna taarifa yoyote iliyowafikia ofisini kwao ya
wanachama wa Taboa kugoma.
“Mimi
niko mkutanoni Morogoro, mkutano wenyewe unahusiana na mambo ya ajali,
hatujapata taarifa rasmi ya wanachama wa taboa kugoma,”alisema Mziray.
MPEKUZI
ilimtafuta Katibu wa Taboa, Enea Mrutu, ili kuzungumzia suala hilo
ambapo alisema kuwa tayari wameshapeleka barua yao Sumatara leo (jana)
saa moja asubuhi na tamko lao ni lilelile waliloadhimia katika mkutano
wao.
“Sumatra
tumekwisha wapelekea barua toka saa moja asubuhi kama wanasema hawana
tarifa wanadanganya kwasababu hata jana katika kikao chetu mwakilishi
wao alikuwepo.
“Ingawaje
kuna taarifa nimeipata kuwa Serikali inataka ifanye mazungumzo na sisi,
tutakaa nao kama wataridhia kuacha nauli kama ilivyokuwa hatuna tatizo
lakini wasipofikia muafaka na kutoa majibu ya kueleweka msimamo wetu
utakuwa ni uleule,” alisema Mrutu.
Wamiliki
wa Mabasi yaendayo mikoani juzi katika mkutano wao walijadiliana juu ya
kushuka kwa nauli na kuafikiana kutoshusha jambo ambalo limetafsiriwa
kuwa ni kuitunishia misuli mamlaka hiyo.
Walisema
endapo Sumatra hawatatoa majibu mapema kuanzia Aprili 29 mwaka huu
(leo) hawatokata tiketi kwa wasafiri na badala yake wataendelea na mgomo
huo kwa siku saba.
Katibu Mkuu wa TABOA, Enea Mrutu, alisema SUMATRA ilikurupuka kushusha nauli bila kufanya mchanganuo na kuda.
Wamiliki
hao waliafikiana kuwa yeyote atakayetoa gari lake kufanya biashara
kabla hawajapata muafaka kutoka SUMATRA watamchukulia hatua za kisheria.
Aidha
waliitaka serikali kurudisha viwango vya nauli za mabasi ya mikoani
kwenye hali yake ya kawaida iliyokuwepo miezi michache iliyopita kwa
sababu bei ya mafuta imerudi juu, baada ya kushuka kwa kisingizio cha
bei ya mafuta kushuka.