Naomba nifafanue kuhusu propaganda inayoenezwa na maafisa wa TCRA kupitia CloundsFM
kuhusu Sikika na Mswada wa #CyberCrimeBill.
Sikika haikuhudhuria mkutano wa wadau unaodaiwa kufanyika Dodoma kama ilivyodaiwa na
Mh Peter Serukamba na leo maafisa wa TCRA.
Sikika haikutoa maoni kuhusu Mswada wa miamala ya kielektoniki kama ilivyodaiwa na Mh
Peter Serukamba na pia leo maafisa wa TCRA.
Sikika ilituma maoni ya pamoja ya wadau kwa niaba ya wadau kuhusu #CyberCrimeBill kwa
njia ya email kwa Mwenyekiti wa Kamati Mh Peter Serukamba.
Maoni hayo hayakutumika kuboresha #CyberCrimeBill bali kuongeza tu orodha ya wadau
wanaodaiwa "kushiriki" kwa lengo la kuonesha kuridhia.
Kwa kuwa maoni ya wadau hayakuzingatiwa na kwamba #CiberCrimeBill iliyopitishwa ina
mapungufu mengi, Sikika na wadau bado wanaipinga.