Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum akisalimiana na mwakilishi kutoka UNICEF katika mkutano wa Lishe mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum akisikiliza kwa makini hoja
iliyokuwa ikitolewa na mwakilishi kutoka CIFF katika mkutano wa Lishe
mjini Washington DC.
Wajumbe kutoka nchi mbali mbali Duniani wakimsikiliza Waziri wa Fedha
Mhe. Saada Salum Mkuya ( hayupo kwenye picha) alipokuwa akiwasilisha
mada na kuchangia hoja mbalimbali katika mkutano uliohusu Lishe bora kwa
mtoto mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum aakitoa mada na kuchangia hoja
mbalimbali zinazohusu Tanzania katika mkutano wa Lishe mjini Washington
DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum akifurahia jambo aliloambiwa na
mwakilishi wa UNICEF baada ya kuchangia mada kuhusu Tanzania, katika
mkutano wa Lishe mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum akipongezwa na Mshauri Lishe wa
Rais Jakaya Kikwete, Dr. Wilbald Lori pamoja na wajumbe kutoka Mataifa
mbalimbali mara baada tu ya kumaliza kuwasilisha Mada kuhusu hali ya
Lishe Tanzania,mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum akipongezwa na Mshauri Lishe wa
Rais Jakaya Kikwete, Dr. Wilbald Lori pamoja na wajumbe kutoka Mataifa
mbalimbali mara baada tu ya kumaliza kuwasilisha Mada kuhusu hali ya
Lishe Tanzania hapa mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum akiulizwa maswali na baadhi ya
wajumbe waliokuwepo kwenye mkutano huo, mara baada tu ya mkutano wa
Lishe mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum akimsikiliza kwa makini mjumbe
aliyekuwa akimuuliza maswali kuhusu hali ya Lishe kwa Tanzania baada ya
mkutano wa Lishe mjini Washington DC.
Lishe bora ni msingi kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi ya nchi.Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya alipokuwa akiwasilisha mada katika mkutano ambao ulikuwa unazungumzia kuhusu suala la Lishe (Nutrition).
"It is important to understand consequences including adverse effects on the child's physical and mental development from conception until it reaches the age of two. These effects are irreversible," he said. "Ni muhimu kuelewa madhara yatakayompata mtoto ikiwa mama hata mnyonyesha mtoto huyo ikiwa ni pamoja na athari mbaya juu ya mwili na maendeleo ya mtoto kutoka mimba mpaka kufikia umri wa miaka miwili kama mtoto hatapat Madhara haya ni kubatilishwa.," Alisema Mkuya.
Mkuya aliongeza kuwa, “ Tanzania tunajitahidi sana kupambana na janga hili kwani mama kushindwa kumnyonyesha mtoto kwa miezi sita kunaweza kusababisha utapiamlo na kusababisha kuathiri mamilioni ya watu katika Tanzania, hasa watoto, na hivyo kusababisha magonjwa kuenea na kunyong’onyesha maendeleo ya kimwili na ki akili”.
“Kwa kuruhusu hali hiyo kunachangia kupunguza uwezo katika kuboresha uwezo wakufikiri, kupunguza nguvu ya kujifunza na kuwa mbunifu, kuongezeka kwa umaskini, na kasi ndogo katika kufikia maendeleo ya kijamii na kiuchumi”.Aliongeza Mkuya.
Takwimu za mwisho za utafiti wa mambo ya afya zina onyesha kuwa asilimia 59 ya watoto wenye umri wa miezi 5-59 wana upungufu wa madini,asilimia 33 ya watoto chini ya miaka sita wana upungufu wa vitamin A. Asilimia 11 ya wanawake wenye umri wa kuzaa yaani miaka 15-49 wana uzito wa chini, asilimia 41 wana uzito wa chini na upungufu wa madini, wakati asilimia 58 ya mama wajawazito wana upungufu wa madini pia.
“Katika Tanzania mikoa ambayo inafanya vizuri katika kupambana na utapiamlo ni mkoa wa Kilimanjaro, Mjini magharibi na Mkoa wa Dar es salaam.” Alisema Mshauri Lishe wa Rais Jakaya Kikwete”.Dr. Wilbald Lori.
Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zinakabiliwa na janga hili, hivyo katika mikutano hii mikakati mbalimbali inapangwa ya jinsi ya kulimaliza kabisa tatizo hili.
Mikutano hii bado inaendelea na hali ya hewa mjini hapa ni baridi kiasi.
Imetolewa na Msemaji :Wizara ya fedha
Ingiahedi C.Mduma
Washington DC
17/04/2015