Kulia
Mkurugenzi wa kampuni ya madini ya Moreshine Gibson A.Kilala akitoa
maelezo kwa Waziri wa nishati na madini George Simbachawene
hivikaribuni jijini Arusha mara baada ya Waziri huyo kutembelea banda
lao katika maonyesho ya nne ya madini na vito yaliyofanyika katika hotel
ya Mount Meru jijini Arusha.
(Habari na Picha kwa hisani ya Pamela Mollel wa jamiiblog) Baadhi ya madini Mkurugenzi wa kampuni ya madini ya Moreshine Gibson A.Kilala akimuonyesha Waziri baadhi ya madini yanayopatikana katika kampuni yao Waziri wa nishati na madini George Simbachawene kushoto akipata maelezo mafupi kutoka kwa mfanyakazi wa Moreshine Bw.William Simba Waziri wa nishati na madini George Simbachawene akiangalia madini. Waziri wa nishati na madini George Simbachawene akiangalia baadhi ya madini yanayopatikana katika banda la Moreshine kushoto ni mkurugenzi wa kampuni hiyo Gibson A.Kilala na kulia ni William Simba mfanyakazi wa Moreshine Bango la Kampuni ya Moreshine. Mkurugenzi wa kampuni ya madini moreshine ya jijini Dar es saalamu Gibson A.Kilala akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)

Changamoto
ya Watanzania kutokuvaa vito vya thamani vinavyotengenezwa na mawe
mbali mbali yanayopatikana hapa nchini imepelekea madini yakiwamo
Tanzanite kukosa soko hapa nchini,Soko la madini haswa tanzanite
limekuwa nje ya mipaka ya Tanzania kwa kuwa watanzania hawana desturi ya
kuvaa madini hayo
Akizungumza
na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Arusha mkurugenzi wa
kampuni ya madini moreshine ya jijini Dar es saalamu Gibson A.Kilala
alisema kuwa kutokuwepo kwa utamaduni huo miongoni mwa watanzania
kumepelekea soko la madini kupatikana nje ya nchi badala ya hapa nchini
ambapo yanapatikana.
Aidha
ameiomba serikali kuweza kusajili kampuni ambayo itasaidia kusafirisha
madini kama zilizo kampuni nyingine za kusafirishia mizigo hapa nchini
kama {DHL)ili kuwawezesha wafanyabiashara kusafirisha mizigo yao kwa
usalama zaidi kama zilivyo nchi za jirani kama Kenya.
Hata
hivyo ameiomba serikali kuondoa changamoto ya mipaka kwa
wafanyabiashara wa madini kwa kuwaruhusu kufuata madini yalipo badala ya
kusubiria brokers hali ambayo inawagharimu muda mwingi lakini pia
gharama kuongezeka.
Amesema
ni vyema wafanyabiashara wakaruhusiwa kwa leseni zao kufuata madini
yalipo ili kuwawezesha kufikia migodini tofauti na sasa ambapo leseni
zao haziruhusu kufuata madini yanapopatikana badala yake kusubiria
broker wawaletee.