Askofu
Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali
Pengo, akiubusu msalaba, wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la
Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam jana, Katikati aliyeshikilia msalaba
huo ni Padri Audax Kaasa wa kanisa hilo.
Mtoto
Benedicta Mushi, ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Masaka English
Medium akiubusu msalaba, wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu, kulia kwa
mtoto huyo ni Baba mzazi Philip Mush.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe, akikomunika
Ekaristi Takatifu katika Kanisa Kuu Katoliki la Mt. Joseph Dar es
Salaam.
Meneja
Miradi Jimbo la Mtama Wilaya ya Lindi, Paul Maokola akibusu mkono wa
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp
Kardinali Pengo, wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la
Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Mtama, mkoani Lindi Bernad
Membe.