Wasanii
wa vichekesho Bongo, Musa Kitale 'Mkude Simba' na Stan Bakola wakiingia
katika ukumbi wa uzinduzi huo wa 4G LTE baada ya kupata maelekezo ya
awali kutoka kwa
wafanyakazi wa Tigo.
Wasanii
wa vichekesho Bongo, Musa Kitale 'Mkude Simba' na Stan Bakola wakiingia
katika ukumbi wa uzinduzi huo wa 4G LTE baada ya kupata maelekezo ya
awali kutoka kwa wafanyakazi wa Tigo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya Huawei wakiuza simu zao katika uzinduzi huo wa Tigo wa netiweki ya 4G LTE.
Ma MC wa sherehe ya uzinduzi huo wakitoa uafafanuzi katika hafla hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tigo Tanzania, Cecile Tiano akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), John Nkoma akielezea namna
ya uboreshwaji wa huduma za mawasiliano nchini unavyoendelea
Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (Mb) akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma hiyo mpya ya 4G LTE
Viongozi mbalimbali wakishudia jinsi netiweki ya 4G LTE inavyofanya kazi katika moja ya skrini
Umati wa watu pamoja na wanahabari waliohudhuria hafla hiyo
KAMPUNI ya mawasiliano ya Tigo imezindua huduma mpya ya kisasa ya ‘internet’ ya 4G LTE ambayo itakuwa ikipatikana nchini.
Uzinduzi
huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam
na kuhudhuriwa na Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa
pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini, Prof. John Nkoma
ambao waliungana kwa pamoja kwenye uzinduzi huo.
Akizungumza
katika uzinduzi huo wa internet ya 4G LTE, Mkuu wa Kitengo cha Internet
wa Kampuni ya Tigo, David Zacharia alisema ‘netiweki’ hiyo ni ya kwanza
kwa Tanzania na kwa mtumiaji wa mtandao huo anatakiwa kuwa na laini ya
4G na simu yenye uwezo wa kupokea 4G, tayari mteja huyo ataweza kupata
huduma hiyo kwa kasi ya ajabu.
Aidha, David alisema mteja ataweza
kunufaika zaidi kutokana na uwezo wa kupokea data haraka, pia uwezo
wake ni mara kumi (10) ya 3G (internet ya iliyozoeleka) na mteja atakaye
kuwa tayari anaweza kujitapatia huduma zote kupitia vituo vyote vya
Tigo kama Mlimani City, Masaki pamoja na maeneo mbalimbali ya Jiji la
Dar.