Utawala
nchini Nepal unasema kuwa watu zaidi ya watu 4000 wamedhibitishwa kuaga
dunia huku wengine 8000 wakijeruhiwa kwenye janga la tetemeko la ardhi
lililosababisha uharibifu mkubwa siku ya Jumamosi.
Tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa wa kipimo cha richta 7.8.
Jitihada
za uokoaji zinaendelea kukiwa na matumaini ya kuwapata manusura, lakini
jitihada hizo bado hazijayafikia maeneo mengine yaliyo mbali.
Watu wengi walilala nje kwa usiku wa tatu mfululizo kwenye mji mkuu Kathmandu wakihofia kutokea kwa mitetemeo mingine midogo.
Serikali
ya Nepal inasema kuwa inahitaji kila msaada ukiwemo wa mablanketi ,
helkopta, madaktari na madereva. Kuna uhaba wa maji , chakula na umeme
huku kukiwa na hofu ya kutokea kwa milipuko ya magonjwa.
Via>>BBC Angalia Picha hali halisi ilivyo
Wafanyakazi wa uokozi kutoka Japan wakiwasili Kathmandu
Hali ya barabara
Watu wakiwa wamelala mitaani baada ya tetemeko la ardhi