Mratibu wa Mradi wa Afya wa Help Kids Edith Peter Mziray akiwasihi wanafunzi kuwa wasikivu wakati wa semina ya Hedhi salama
Mkurugenzi
mtendaji wa Kasole Secrets Hyasintha Ntuyeko
ambao pia ni waandaaji wa siku ya Hedhi Duniani kwa Tanzania akiwauliza
wanafunzi wa Darasa la tano hadi la saba changamoto wazipatazo wakati
wanapoingia katika siku zao na pia kuwaelimisha juu ya Hedhi salama.
Mwanafunzi
wa Darasa la Tano Anitha Norbart (12) akiuliza swali kama ni sahihi
kutumia Mdalasini wakati akiwa katika siku zake?
Daktari
Edna Kiogwe akitoa elimu juu ya umuhimu wa kujitambua wakati wakiwa
katika Hedhi na njia mbadala za kujiweka sawa pindi wanapokuwa katika
kipindi hicho
Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia kwa Makini Semina Hiyo
Mmoja
wa wanafunzi wa shule ya Msingi ya Bajavero akipewa zawadi ya Glory
Pads ikiwa ni sehemu ya kusherekea siku ya Hedhi Duniani.
Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Bajavero zamani Wamato wakifurahia Pads za
Glory walizopewa ikiwa ni ishara ya kusherehekea sikukuu ya Hedhi
Duniani.
****
Kuelekea Kilele cha siku ya Hedhi Duniani ambayo itakuwa tarehe 28.05.2015 Mtandao wa Hedhi salama www.hedhisalama.com
umeendelea kutoa mafunzo juu ya Hedhi salama ikiwa ni pamoja na
changamoto,Magonjwa na mambo mbalimbali ambayo yanamtokea mwanamke
anapokuwa katika Hedhi pamoja na ushiriki wa wanaume katika kujua
maswala ya hedhi katika shule ya msingi ya yatima ya Bajavero,
Akitoa mafunzo ya Semina hiyo Daktari Edna
Kiogwe alieleza kuwa kuna haja ya vijana tangu wakiwa wadogo wakapata
Elimu juu ya Hedhi ili wanapokuwa wasijeshtuka pindi hali hiyo inapo
wajia.
Alieleza
juu ya umakini na ufaulu mashuleni kuwa Wasichana wengi huahirisha
shughuli za kimasomo kama kuhudhuria vipindi mbalimbali vya masomo yao
Aliongeza ili Binti apate kuendana na hali hii anatakiwa ajivunie na
kufurahia kipindi chote anachokua hedhi, atambue kwamba kila mwanamke
hupitia kipindi hicho na hata wenzake darasani huvipitia vipindi hivyo
vya hedhi, si yeye
peke yake anaeingia hedhi.
Pia Dkt. Edna alisisitiza kuwa Wanaume na wavulana wanahitajika
kuelimishwa juu ya hedhi, wengi wao hawajui chochote juu ya hedhi na hua
wanadhani mwanamke peke yake ndo anapaswa kufahamu juu ya hedhi.
"Tukiwaelimisha wanaume juu ya hedhi, watakua msaada mkubwa kwa wake
zao, watoto wao, dada zao,mama zao na ndugu zao wa kike. Kulingana na
tamaduni zetu za kiafrika baba ndo mtafutaji na mwenyekauli ya mwisho
katika familia" Alisema Dkt. Edna
Nao wanafunzi wa shule ya msingi ya Bajavero
walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali na kupata majibu pia
kufurahishwa na elimu bora na kujitambua zaidi, pia walishukuru kupata
zawadi za Pads aina ya Glory ikiwa ni kuelekea katika siku ya Hedhi
duniani.