Waziri
wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Mkoani Geita,
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapongeza wanafunzi wa kidato cha
Sita katika Shule ya Sekondari ya Chato wanaotarajiwa kuhitimu masomo
yao mwezi ujao.
Wanafunzi
wa kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Chato Mkoani Geita
wanaotarajiwa kuhitimu masomo yao mwezi ujao wakiimba wimbo maalum wa
Shule hiyo katika Mahafali ya 10 shuleni hapo.
Waziri
wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akimkabidhi cheti mwanafunzi mmojawapo katika mahafali
hayo.
Waziri
wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akiangalia kazi ya uchanaji wa mbao katika Shule ya
Sekondari Chato. Mbao hizo hutumika katika kazi mbalimbali za ujenzi wa
shule hiyo. Pia Dkt. Magufuli ameichangia shule hiyo kiasi cha Shilingi
Milioni tano.
Waziri Magufuli akikagua moja ya computer katika shule hiyo.kushoto kwake ni Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Mahendeka Mafele.
Dkt. Magufuli akipiga ngoma pamoja na kikundi cha Skauti cha Shule ya Sekondari Chato kabla ya kuanza kwa mahafali hayo.
Waziri
wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akikagua vifaa katika maabara ya shule hiyo.
Waziri
Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Chato
Mwalimu Mahendeka Mafele kuhusu Ujenzi wa vyoo unaoendelea.
baadhi ya wazazi waliohudhuria katika mahafali hayo ya kumi ya kidato cha Sita shuleni hapo.
Vijana
wanaotarajiwa kuhitimu kidato cha sita katika shule hiyo wakitoa
burudani pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya Shule hiyo Bi Helena Busumilo.