Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa
CITI na Mkuu wa Afrika kwa kundi la sekta ya utumishiwa umma Bw. Peter
M. Sullivan alipo mtembelea Mhe.Waziri kwa madhumuni ya kuisadia nchi ya
Tanzania katika ubalozi wa Marekani mjini Washington DC.
Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya wa katikati akiwa pamoja na ujumbe
kutoka Tanzania walipokutana na Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya
Afrika sehemu ya Mashariki Bw.Herve’ Joly walipokuwa wakijadiliana na
kuangalia ni jinsi gani Tanzania imeweza kutekeleza sera za Shirika la
fedha la Kimataifa mjini Washington DC.
Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akimsikiliza kwa makini Bi. Diana
Layfield ambaye ni Mtendaji mkuu wa kanda ya Afrika, alipokuwa akieleza
mambo ambayo Standard Chartered inaweza kuyafanya katika kuendeleza
uchumi wa Tanzania mjini Washington DC.
Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akimsikiliza kwa makini Bw. Atlas
Mara co-Founder, Ashish. J. Thakkar alipoomba kukutana naye ilikuweza
kuangalia jinsi anavyoweza kuja kuwekeza katika nchi ya Tanzania.Mkutano
huo ullifanyika mjini Washington DC.Wengine ni wajumbe kutoka nchini
Tanzania.
Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya alipokutana na Makamu wa Rais JICA
anayesimamia nchi za Afrika, Bw. Kato Hiroshi na Bw. Kiyoshi Kodera
ambaye ni Makamu wa Rais kiongozi katika Benki ya Dunia, walipokuja
kuelezea nia yao ya kutaka kuendelea kuleta miradi nchini Tanzania.
Maongezi hayo yalifanyika katika ukumbi wa ubalozi wa Marekani mjini
Washington DC.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius
Likwelile akiongoza kikao cha mradi wa kufadhili uwekezaji nyumba.
Anayetoa maelezo ni Bw. Baraka kutoka Benki kuu katika mradi huo.
Mkutano huo ulifanyika mjini Washington DC.
Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile walipokuwa na Naibu
katinu Mkuu Marekani Bw. W.L. Mc Donald nje ya jengo la Hazina
Marekani.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius
Likwelile na ujumbe kutoka Tanzania walipokuwa wakifanya mkutano wa moja
kwa moja kutoka Tanzania na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali. Kama
wanavyoonekana kwenye kivuli cha Runinga.Mkutano huo unafanyka Mjini
Washington DC. Na Dar es salaam Tanzania.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius
Likwelile na ujumbe kutoka Tanzania walipokuwa wakifanya mkutano wa moja
kwa moja kutoka Tanzania na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali.
Hawapo kwenye picha.Hapa walikuwa wanajadiliana ili wote
waafikiane.Mkutano huo unafanyka Mjini Washington DC. Na Dar es salaam
Tanzania.
(Picha zote na Ingiahedi Mduma Washington DC.)