Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (wa
pilikulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Balozi Juma Mwapachu
(wapili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso (kulia) na
Menejawa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi wakiwa wameshika bango
kamaishara ya uzinduzi wa mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’, katika
haflailiyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti
Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (wa pili kulia),
akikabidhi zawadi ya pasi na meza yake kwa muuza mitumba RashidSeleman
(wa pili kushoto), ambaye ni mmoja wa vijana waliowezeshwa na mpango wa
Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’ katika hafla ya uzinduzi wa mpango huo,
iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji
wa Airtel Sunil Colaso, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Balozi
Juma Mwapachu (wa tatu kushoto) na Meneja wa Huduma kwa Jamii wa
Airtel, Hawa Bayumi.
Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (wa
pili kulia), akikabidhi zawadi ya mashine ya kutengeneza juisi kwa
Abdulkarim Ramadhan (wa tatu kushoto), ambaye ni mmoja wa vijana
waliowezeshwa na mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’ katika hafla ya
uzinduzi wa mpango huo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka
(kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso, Mwenyekiti wa
Bodi ya Airtel Tanzania, Balozi Juma Mwapachu na Meneja wa Huduma kwa
Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi akizungumza katika
hafla ya uzinduzi wa mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’,
iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Airtel Tanzania, Balozi Juma Mwapachu akizungumza katika
hafla ya uzinduzi wa mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’,
iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
uzinduzi wa mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Baadhi ya vijana waliohudhulia katika hafla ya kuzindua Program mpya iitwayo Airtel Fursa , wakisalimiana na Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi jana jijini Dar es Salaam.
AIRTELTanzania imezindua programu mpya iitwayo Airtel Fursa itakayowawezesha vijana kiuchumi ikiwemo kuwapa mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kupata maendeleo zaidi katika shughuli zao.
Akizungumza katika uzinduzi wa programu hiyo, Mgeni wa heshima na mfanyabiashara mkubwa nchini Dokta Reginald Mengi aliipongeza Airtel kwa kubuni program hiyo itakayosaidia vijana nchini huku akitoa wito kwa vijana wote nchini kuikumbatia fursa hiyo ili kuweza kutimiza malengo yao.
“Hii ni Fursa ambayo vijana wanatakiwa kuikumbatia kwa nguvu zote ili wale wote watakaofaidika waweze kuwashawishi wenzao pia katika miaka ijayo,” alisema”
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso alisema vijana watanufaika kwa njia mbalimbali na wataweza kujiendeleza kiuchumi na kupunguza suala la ukosefu wa ajira.
“Airtel FURSA itawawezesha vijana toka sehemu mbalimbali nchini, Fursa zitawafikia vijana wengi wenye kiu na ari ya kufanya ambacho wanakiamini na ambao wako tayari kukabili changamoto mbalimbali ili waweze kufikia malengo yao na kubadilisha hali yao kimaisha,” alisema Colaso.
Alisema program hiyo inawalenga vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 ambao watapokea misaada ya vifaa au thamani ili kuweza kutimiza malengo yao.
Mbali na kutoa vifaa hivyo, Bw, Colaso alisema zaidi ya vijana wapatao 1500 watapata mafunzo mbalimbali ya kibiashara kila mwaka kupitia program hiyo.
“Watafundishwa kuhusu usimamizi bora wa fedha, namna ya kupata mikopo, namna ya kufugua akaunti benki na mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa biashara,” alisema Colaso.
Alisema program hiyo itahusisha vijana kutoka Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya na Mtwara.Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Airtel Balozi Juma Mwapachu, aliwataka vijana kutumia program hiyo ya Airtel Fursa kujiendeleza. Huku akiwaomba watanzania kuwapendekeza vijana wote wanaoona wanafaa kufaidika kwa mradi huo kwa manufaa ya jamii zao.
Ili kijana kushiriki au kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- JIna, Umri, aina ya biashara na eneo.
Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com. ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, aina ya biashara na sababu ya kuomba msaada kutoka Airtel.
Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.com.
“Programu hii itanufaisha vijana ambao tayari wana miradi mbalimbali na sio ambao wanataka kuanzisha,” alisema.