Kundi la Dola ya Kiislam (IS)
limeutwaa mpaka wa Syria na Irak uliokuwa chini ya serikali ya Syria,
taarifa iliyotolewa na kundi linalofuatilia mgogoro wa nchi hiyo
imesema.
Kundi hilo la Uangalizi wa Haki za
Binadamu Syria limesema vikosi vya serikali vimejitoa kutoka katika
mpaka wa al-Tanf uliopo Homs, wakati wapiganaji wa IS wakisonga
mbele.
Kutwaliwa kwa mpaka wa al-Tanf
inafuatia kundi la IS kuutwa mji wa kale wa Palmyra siku ya jana.
Marekani imesema kupigana wapiganaji wa IS ni changamoto ngumu.
Kundi la Dola ya Kislam sasa
linashikilia eneo la kilomita mraba 95 la Syri ambalo ni sawa na
asilimia 50 ya eneo lote la taifa hilo.