Wapiganaji wa Kundi la Dola ya
Kiislam (IS) nchini Syria wameutwaa mji wa kale wa Palmyra na
wameingia kwenye eneo la mabaki ya majengo ua kale yenye thamani.
Kundi linalofuatilia hali ya Syria
limesema hakuna ripoti yoyote hadi sasa kuhusu uharibifu wa majengo
hayo ya kale.
Kundi la IS pia linashikilia uwanja
wa ndege uliokaribu, gereza pamoja na makao makuu ya idara ya
ujasusi. Serikali imekiri kuondoa vikosi vyake katika mji huo.