Mkurugenzi
wa halmshauri ya wilaya ya Ruangwa, Nicholous Kombe (kulia) akikabidhi mfano wa
hundi yenye thamani ya sh milioni 100 kwa Mwenyekiti wa WAALIMU SACCOS ya
Ruangwa, Hamisi Malunga (kushoto) ikiwa ni mkopo uliotolewa na mfuko
wa pensheni wa LAPF kwa wanachama wa SACCOS hiyo. Katikati yao ni Meneja
wa LAPF, Kanda ya mashariki, Yessaya Mwakifulefule pamoja na wanachama wa
Saccos hiyo wakati wa mabidhiano hayo juzi Wilayani Ruangwa mkoani Lindi.
Wanachama
wa Walimu Saccos wa Wilaya ya Ruangwa mkoani
Lindi wakifurahia mkopo wenye thamani
ya shilingi Milioni 100 uliotolewa na Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwa wanachama
wa Saccos hiyo. Anaeshuhudia wa pili kulia ni Meneja wa LAPF, Kanda ya Mashariki,
Yessaya Mwakifulefule. Hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika Wilayani Ruangwa hivi
karibuni.
***************
Mfuko wa pensheni wa LAPF leo umetoa mkopo wenye thamani ya shilingi
milioni mia moja kwa Saccos ya waalimu iliyopo wilayani ruangwa mkoani Lindi.
Akipokea hundi ya mkopo huo kwa kwa niaba ya wanachama wa Waalimu
Saccos,mkurugenzi wa halmshauri ya Ruangwa Bw Nicholous Kombe aliishukuru mfuko
wa LAPF kwa kuwajali na kuwawezesha wanachama wa SACCOS hiyo ambao walikua
wakiuhitaji sana mkopo wa aina hiyo.
Akishukuru kwa niaba ya waalimu wanachama wa saccos hiyo,Mwenyekiti wa
saccos Bw Hamisi Malungu aliwaomba wanachama wake wadumishe nidhamu na
kuheshimu kulipa mikopo yao kwa wakati ili Saccos yao iweze kukopesheka Zaidi.
Nae Meneja wa LAPF kanda ya mashariki Bw Yessaya Mwakifulefule,aliwapomgeza
wanachama wa SACCOS hiyo na kuwashauri waalimu wengi Zaidi wachague kuchangia
makato yao kwa mfuko wa LAPF ili na wao waweze kufaidika na mikopo kama hiyo li
waweze kuwajikwamua kiuchumi.
Aidha bwana Mkwakifulefule alisema mpaka sasa LAPF imesha kopesha Zaidi
ya shilingi bilioni mbili kwa saccos mbali mbali za wanachama ambao makato
yao wanachangia ktk mfuko huo hapa nnchini.
Waalimu SACCOS ilianzishwa mwaka 2001 ikiwa na wanachama 60 ambapo
mpaka sasa saccos hiyo ina wanachama Zaidi ya 300 na hisa zenye thamani ya
shilingi 26,000,000.