Kingine ambacho nimeona nikusogezee leo MAY 21 2015 ni huu uchambuzi wa Stori za Magazetini.
Stori kubwa ni kuhusu siku ya leo ambayo ni kumbukumbu ya ajali ya meli ya MV Bukoba
ambayo ilipata ajali mwaka 1996.. Kwenye zilizochambuliwa iko pia stori
ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU amesema uchunguzi unaanza kwa wahusika
wa ubadhilifu wa fedha za umma kutokana na Ripoti ya CAG, Mwigulu Nchemba amesema Serikali imeshatoa fedha za wanafunzi wa Vyuo Vikuu TZ.
Ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu
imesema Jeshi la Polisi lilitumia nguvu kuwakamata viongozi wa CUF na
wanachama wake Mbagala, watu wa Dar wako hatarini kupata magonjwa
mbalimbali kutokana na nyama inayochinjwa kutopimwa.
Hospitali ya Rufaa Mbeya imepiga
marufuku ‘wanaovaa ovyo’ kuingia Hospitali hiyo, Mbunge wa Rombo
amewajia juu Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro ameunda Tume kuchunguza sakata la
Mtumishi aliyesimamishwa kazi KCMC kwa kumtumia message Rais JK,
nyingine inatokea Rombo ambapo Mbunge wa Jimbo hilo amemjia juu Mkuu wa
Wilaya kujiuzulu kutokana na kushindwa kuwajibika baada ya kuandiikwa
stori kwamba wanawake wa Rombo wanakodi wanaume toka Kenya ili wafanye
nao tendo la ndoa.