Msemaji wa Simba ambaye
ameambatana na Taifa Stars Afrika kusini, Hajji Sunday Manara anasema:
“Nilibahatika kwenda ‘dressing room’ ya team ya Madagascar, kuwapongeza
na walifurahi sana kupiga picha na Mtanzania hata baada ya kutufunga.
“Ila kiukweli kocha wetu ni Bomu kupita Bomu. Nikirudi Bongo nitaongoza kampeni ya kitaifa kumuondoa”.
Hajji Manara (kulia)
“Sikutegemea hata baada ya
kufungwa mbili angeweza kufanya sub ya hovyo namna ile.Maana hatukuwa na
cha kupoteza tena. Hakupaswa kuingiza defender na kumtoa kiungo wa
ushambuliaji. Yaani kocha ni Bomu kupita kiasi
“Amechukua wachezaji ambao hata kwenye team zao hawapati namba. Bocco nitajieni kacheza game ngapi za Azam?