Pacquiao anaweza kuwa nje ya ulingo kwa zaidi ya miezi tisa, wakati anajiandaa kwenda kufanyiwa upasuaji wa bega baada ya kuumia mazoezi akijiandaa na pambano hilo.
Ushahidi wa nakala ya fomu iliyotakiwa kujazwa na bondia huyo kutoka Ufilipino umetolewa na inaonyesha katika kipengele cha majeraha hakikujazwa huku ikionyesha Pacquiao alitumia dawa kadhaa za maumivu.
Sehemu muhimu inayothibitisha uweli wa jambo hilo imezunguushiwa mstari mwekundu kwa ushahidi, ambapo swali liliuliza; ‘Ulikuwa una maumivu yoyote kwenye mabega yako, chini ya mabega, au mikononi ambayo yanahitaji vipimo vya uthibitisho wa kupona?’

