RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIWA NA MAFURIKO JIJINI DAR ES SALAAM
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo amekagua baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa
vibaya na mafuriko jijini Dar es Salaam na kuwapa pole wakazi wa maeneo
hayo.
Maeneo
aliyotembelea Rais leo ni Mbagala Mwanamtitu na Daraja la Msimbazi
ambapo amejionea uharibifu uliofanywa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Pichani
Rais Kikwete akiangalia Darala la Mwanamtitu Mbagala lililosombwa na
maji na daraja la muda la miti lililojengwa na wakazi wa Eneo hilo na
kisha kuwapa pole kwa adha wanazozipata
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa maelekezo kwa mhandisi wa TANROADS
kutoa uchafu ulijaa chini ya daraja la Msimbazi eneo la Jangwani.
Rais Dkt..Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Daraja la mto Msimbazi Eneo la Jangwani wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo.