https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    TASWIRA TUZO ZA WATU 2015

    IMG_0917Millard Ayo na Salim Kikeke
    Tuzo za watu 2015 zimetolewa Ijumaa hii kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa ‘surprises’ za kutosha. Mshindi mkubwa kwenye usiku huo na ambaye amekuwa surprise kwa wengi ni mtangazaji wa TBC FM, D’jaro Arungu aliyeibuka na tuzo mbili.D’Jaro alikuwa akishindana na Millard Ayo kwenye vipengele hivyo viwili ambaye hata hivyo alishinda pia kipengele cha blog inayopendwa.
    IMG_0770D’Jaro Arungu akiongea baada ya kutangazwa mshindi
    “Mtu yeyote aliyekuwa anashindani halafu anaamini anaweza kupata nafasi lazima imshtue,” Millard ameiambia Bongo5.
    IMG_0789Millard Ayo akipokea tuzo ya blog inayopendwa
    “Lakini inakushtua kwa njia nzuri kwamba kuna kitu kimemiss au labda unatakiwa ufanyie kazi zaidi. Lakini pia kura zinamata, inachangia sehemu zote, inawezakana ubora wa kipindi na kura pia. Lakini all in all mimi nampongeza sana D’Jaro Arungu, ameshinda kura zote mbili, ni changamoto pia, inatupa nafasi sisi wenyewe kushindana lakini inasaidia pia kufanya kazi kwenye biashara yetu vizuri.”
    Wema Sepetu aliyekuwa ametajwa kuwaniwa vipengele vitatu ameibuka na tuzo moja.
    IMG_0818Wema Sepetu akipokea tuzo yake ya muigizaji wa filamu anayependwa
    “I’m Grateful… I’m humbled…. I’m out of words… Ila nawapenda for making this happen…. Shout out to all my fans out there… Na haters pia…. I say it’s a new beginning.”
    IMG_0813
    “Therez more to this…. I take it as a challenge and a wake up call to give you guys more of what you want me to give,” ameandika Wema kwenye Instagram baada ya ushindi huo,” aliongeza Wema.
    IMG_0792 Ray akishukuru baada ya kutangazwa mshindi wa kipengele cha muongozaji wa filamu anayependwa
    IMG_0767Salim Kikeke
    IMG_0738Dada wa Alikiba akipokea tuzo kwa niaba ya kaka yake
    IMG_0746
    IMG_0730Lady Jaydee akishukuru baada ya kushinda tuzo ya mwanamuziki wa kike anayependwa
    IMG_0712Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamanzima akimkabidhi tuzo Ommy Dimpoz
    IMG_0841
    Nancy Sumari akiwapongeza washindi
    IMG_0836Luca Neghesti na Nancy Sumari wakifurahia kilele cha tuzo za watu
    IMG_0831Shangwe kwa washindi
    IMG_0832
    IMG_0825
    IMG_0688Jacqueline Mengi na Nasreen Karim ni miongoni mwa waliohudhuria
    IMG_0686 Joh Makini na Salim Kikeke
    IMG_0682 Mtu na binamu yake: Wakazi na Lady Jaydee
    IMG_0680
    IMG_0672
    IMG_0664Luca na Nancy wakizungumzia tuzo za watu 2015

    Hii ni orodha kamili ya washindi
    Mtangazaji wa redio anayependwa
    D’Jaro Arungu – TBC FM

    Kipindi cha redio kinachopendwa
    Papaso – TBC FM

    Mtangazaji wa runinga anayependwa
    Salim Kikeke – BBC Swahili

    Kipindi cha runinga kinachopendwa
    Mkasi – EATV

    Blog/Website inayopendwa
    Millardayo.com

    Muongozaji wa video anayependwa
    Hanscana

    Muongozaji wa filamu anayependwa
    Vincent ‘Ray’ Kigosi

    Muigizaji wa kike wa filamu anayependwa
    Wema Sepetu

    Muigizaji wa kiume wa filamu anayependwa
    Hemedy PHD 

    Mwanamuziki wa kike anayependwa
    Lady Jaydee

    Mwanamuziki wa kiume anayependwa
    Alikiba

    Filamu inayopendwa
    Kigodoro

    Video ya muziki inayopendwa
    Nani kama Mama – Christian Bella f/ Ommy Dimpoz
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: TASWIRA TUZO ZA WATU 2015 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top