Hisa katika soko la mataifa la Ulaya
pamoja na paundi ya Uingereza zimeongezeka thamani kwa kasi baada ya
matokeo ya uchaguzi kuonyesha chama cha Conservatives kimepata
ushindi mkubwa.
Hisa za makampuni mbalimbali ya
nishati na mabenki zimepanda katika soko la hisa kufuatia matokeo
hayo.
Pia katika soko la fedha paundi
ya Uingereza imeongezeka thamani dhidi ya dola ya Marekani.