Waandamanaji wawasha vizuizi vya barabara mjini Bujumbura
Serikali
ya Burundi imewaagiza waandamanaji katika mji mkuu wa Burundi Bujumbura
kusitisha maandamano yao dhidi ya hatua ya rais wa taifa hilo Pierre
Nkurunziza kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi wa mwezi ujao.
Mamlaka imewapatia waandamanaji hao saa 48 kuondoa vizuizi walivyoweka katika barabara za mji huo.
Hakuna
maandamano yanayoendelea leo kufuatia vifo vya waandamanaji wawili
lakini waandalizi wake wamesema kuwa maandamano yataendelea siku ya
jumapili.
Waandamanaji
wawasha vizuizi vya barabara mjini BujumburaWaandalizi wanasema kuwa
bwana Nkurunziza anakiuka katiba kwa kuwania muhula wa tatu,lakini
mapema wiki hii mahakama ya kikatiba nchini Burundi iliamua kuwa rais
Nkurunziza ana haki ya kuwania muhula wa tatu.
Takriban watu 18 wameuawa tangu maandamano hayo yaanze wiki mbili zilizopita.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako

