Timu ya taifa ya Argentina imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Uruguay katika mechi ya pili ya kundi B la michuano ya mataifa ya America kusini, Copa America inayoendelea nchini Chile.
Bao pekee la Argentina chini ya kocha Tata Martino limefungwa na Sergio Kun Aguero katika dakika ya 56′.
Goli hilo limetokana na Manchester City kwasababu Pablo Zabaleta aliambaa na mpira kutoka winga ya kulia na kujaza krosi murua iliyotua kichwani kwa Aguero aliyecheka na nyavu.
![Argentina manager Gerardo Martino is sent to the stands in the first half after an argument with the Brazilian officials](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_tAISg985HV7_cU28LzpIcqsdD5gjtU_630WCQpJR15GV1jVCJJjm4IdkxZrXg_PwbqgMQQKbF8gO2DiiR1FfRM_6Ujc_OQJgzBBBx0bmYf0_VCWsv4Fzw8hAxGmZiu2JRHcrnSutqF-dud0wjLuaKxqtEAq1AaXXjSc7lAIbPum5EVQfxI=s0-d)
Hata hivyo mechi hiyo ilikuwa na upinzani mkubwa ambapo kocha Martino alitolewa kwa kadi nyekundu katika kipindi cha kwanza baada ya kuzozana na mwamuzi wa mechi.
Hata hivyo mechi hiyo ilikuwa na upinzani mkubwa ambapo kocha Martino alitolewa kwa kadi nyekundu katika kipindi cha kwanza baada ya kuzozana na mwamuzi wa mechi.
Mechi nyingine ya kundi B, Paraguay imeinyuka Jamaica kwa bao 1-0 .
Edgar Benitez ameifungia Paraguay goli la ushindi katika dakika ya 36′.