Mchezaji aliyetokea benchi, Thomas
Partey amefunga bao la ushindi la dakika za mwisho dhidi ya Levante
na kuipashia Atletico Madrid kuongoza Ligi ya Kuu ya Hispania ya La
Liga.
Atletico imepata fursa hiyo ya kukaa
kileleni kufuatia Barcelona kutoa sare tasa ya 0-0 dhidi ya
Espanyol, na kuongoza kwa pointi mbili ikiwa imecheza mchezo mmoja wa
ziada.
Mabingwa hao wa Ligi hiyo mwaka
2013-14 walionekana kama watachanganyikiwa katika mchezo huo, baada
ya Koke kupiga mwamba wa juu wa goli kwa shuti kali la umbali wa yadi
20.
Hernan Perez akimvuta jezi Lionel Messi katika mchezo wa jana
Kipa Pau Lopez akimyima bao Luis Suarez katika mchezo huo wa jana
Lionel Messi na Neymar wakifunika nyuso zao kwa majonzi
0 comments:
Post a Comment