Meya mpya mwanamke nchini Mexico
amepigwa risasi na kufa katika siku yake ya pili tangu aingie
madarakani.
Meya Gisela Mota ameuwawa nyumbani
kwake katika mji wa Temixco, kilomita 85km kusini mwa mjii Mkuu wa
Mexico City, ikiwa ni saa chache kupita tangu alekiapo siku ya
Ijumaa.
Taarifa zimeeleza kuwa alishambuliwa
na wanaume wanne wenye silaha, polisi wamefanikiwa kuwa kamata
washambuliaji wawili na kuwauwa wengine wawili.
Chanzo cha mauaji hayo
hakijajulikana, ingawa mameya kadhaa Mexico waliuwawa mwaka jana na
magenge ya wasafirishaji dawa za kulevya.
0 comments:
Post a Comment