Mwishoni mwa Juma lililopita, nyota wa Arsenal, Mesut Ozil alikuwepo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kilichoichapa Gibraltar kwa goli 7-0 kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya (Euro 2016).
Jumapili, Ozil aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akidai kwamba ni muda wa kupumzika kwa wiki kadhaa baada ya kumaliza msimu wa mechi za kimataifa.
Kiungo huyo wa Ujerumani ameonekana kuachia nywele zake kidogo tofauti na alivyozoeleka.
Wakati anatoka kwenye klabu ya Los Angeles alipoenda kula bata, Ozil alipigwa picha, lakini alionekana kutopenda kufanyiwa hivyo.
Nyota huyo wa zamani wa Real Madrid akijaribu kuficha sura yake wakati anatoka Hooray Henry alipoenda kula bata.
Ozil alificha kabisa sura yake ambapo alikaa kiti cha mbele na mwanaume mmoja na nyuma yake kulikuwa na watoto wazuri wawili.