FC Barcelona wameliondoa jina la Luis Figo kwenye orodha ya
kikosi chao cha magwiji wa klabu hiyo kitakachopepetana na magwiji wa
Juventus kesho jumamosi kabla ya mechi ya fainali ya Uefa Champions
League itayopigwa mjini, Berlin, Ujeruman.
Figo alialikwa na UEFA kuiwakilisha Barcelona na baada ya Barca kugundua hilo wamelitoa jina lake.
KWANINI?
Kwasababu Figo hachukuliwi kama gwiji Camp Nou wakidai
aliondoa heshima hiyo baada ya kujiunga na wapinzani wakubwa wa
Barcelona, Real Madrid.
Figo alianza kujiimarisha kuwa gwiji Barcelona katika miaka
mitano aliyokaa Camp Nou, lakini kuondoka kwake kuliharibu kila kitu.
Alipoondoka Barcelona na kujiunga na Real Madrid,
hakuheshimika tena Katalunya na alipokuwa anarudi kucheza mechi za El
Clasico, mashabiki walikuwa wanampokea kwa hasira.
Figo alichukuliwa kama msaliti kwa Barcelona, alienda kwa
wapinzani wao wa jadi, Madrid, ambapo alishinda makombe ya Uefa
champions League.