Mwanariadha
wa Marekani, Justin Gatlin amevunja rekodi iliyowekwa na Usain Bolt na
kuweka rekodi mpya katika mbio za Diamond League za mita 100.
Gatlin mwenye umri wa miaka 33
anayeishi huko Orlando, Florida, aliwaongoza wenzake kushinda kwa
sekunde 9.75 ikiwa ni muda bora wa saba kuwekwa katika historia na
ameipiku rekodi ya Bolt (lightning Bolt) ya sekunde 9.76 iliyoweka mwaka
wa 2012.
Gatlin ambaye amepigwa marufuku
kutumia dawa za kusisimua misuli alikimbia mda wa sekunde 9.74 katika
mkutano wa kwanza wa mbio za Diamond League mwezi uliopita.
Bingwa wa mbio za Olimpiki
Sally Pearson alipata jeraha la kifundo cha mkono baada ya kuanguka
katika mbio za kuruka viunzi za mita 100 upande wa wanawake.