Afisa habari wa klabu ya Simba Hajji Manara amesema, Simba wamempa baraka zote kiungo huyo licha ya kuwa ameitwa kwenye timu ya Taifa, Manara amesema tayari wamezungumza na kocha wa Stars Boniface Mkwasa kumpa taarifa hiyo ya kiungo wao anaekwenda kufanya majaribio ya siku 14 (wiki mbili).
“Tumempa baraka zote za kwenda kufanya ‘trial’ lakini kumalizana naye ni mpaka hapo badae atakapofuzu lakini tumempa baraka zote ‘full’, amepata ‘support’ ya Simba”, amesema Manara.
“Ni kweli Mkude ameitwa kwenye timu ya Taifa lakini Mungu jaalia tumeshazungumza na coach Charles Boniface Mkwasa na kumpa taarifa hiyo kwamba Jonas anaondoka na yeye alikuwa hana taarifa hiyo lakini nadhani haitakuwa tatizo kwake kwasababu anachoenda kukifanya pia ni nsehemu ya ‘program’ za TFF, lazima tuongeze ‘professionals’ wengi zaidi nadhani ni baraka kwa nchi, wal Boniface hatakuwa na shida, ni mwalimu mweledi sana”, ameeleza.
“Anakwenda Wits University jina lao la utani wanaitwa ‘The clever boys’ ilishika nafasi ya tatu nadhani kwenye msimu uliopita, atafanya majaribio ya siku 14 pale”, alimaliza Manara.

