https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    PAPAA MSOFFE AFUTIWA KESI YA MAUAJI, AFUNGULIWA NYINGINE YA KUGHUSHI NYARAKA


    Papaa Msofe akiwa mahakamani. (Picha kutoka maktaba yetu)
    MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imemfutia kesi ya mauji iliyokuwa ikimkabili mfanyabishara maarufu nchini, Marijan Abubakar, maarufu kama ‘Papaa Msofe’ baada ya kupokea taarifa kutoka kwa MKurugenzi wa Mashitaka (DPP), Biswalo Mganga leo kuwa hana nia ya kuendelea kumshitaki tena.
    Kwa mujibu wa Kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, inampa mamlaka DPP kuifuata kesi ya jinai bila kuhojiwa na mtu yeyote wala mamlaka yoyote ile.
    Hata hivyo dakika chache baada ya kufutiwa Kkesi hiyo ya mauaji kinyume na Kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka 2002 ambapo kisheria Mahakama ya Kisutu ilikuwa haina mamlaka ya kuisikiliza na haina dhamana na hivyo kwa Kipindi chote hicho tangu Agosti 10, mwaka 2012 hadi leo alikuwa akiishi Gereza la Keko kabla ya kuhamishiwa Gereza la Ukonga, Dar.
    Mara baada ya kufutiwa kesi hiyo, upande wa Jamhuri ulimfungulia kesi nyingine ya kughushi nyaraka za viwanja ambayo endapo akitimiza masharti ya dhamana atapata dhamana yake na hivyo kurudi nyumbani kwake kuungana na familia yake.
    Mpaka mwandishi wa habari hii anaondoka eneo la mahakama Papaa Msofe alikuwa bado hajatimiza masharti ya dhamana na bado alikuwa chini ya ulinzi katika eneo la mahakama hiyo.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: PAPAA MSOFFE AFUTIWA KESI YA MAUAJI, AFUNGULIWA NYINGINE YA KUGHUSHI NYARAKA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top