https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Mkulima atumia mabasi kusaka wadhamini


     Kada wa CCM, Elidephonce Bilohe (43), mkulima anayeomba kupitishwa na chama chake kuwania urais, amesema anatumia usafiri wa mabasi ya umma kuzunguka mikoani kusaka wadhamini.
    Wakati Bilohe akitumia usafiri huo, wagombea wenzake wanatumia au walitumia mabasi waliyokodi na kuyafanyia maboresho ndani, magari madogo na ndege kutafuta wadhamini 450 kutoka mikoa 15 inayotakiwa kwa mujibu wa taratibu za CCM.
    Akizungumza na Mwananchi jana, Bilole alisema ameshafika mikoa tisa ambayo ni Dodoma, Kigoma, Geita, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Tabora, Morogoro na Dar es Salaam, tangu alipochukua fomu hiyo Juni 9.
    “Huko kote nimekuwa nikienda kwa kutumia usafiri wa mabasi ya abiria na daladala. Kwa kweli nimepata ushirikiano mzuri kutoka kwa makatibu wa CCM, nawashukuru sana,” alisema.
    Bilohe alisema atakwenda mikoa 15 tu kama inavyotakiwa na chama chake, tofauti na watiania wengine ambao baadhi wamekwenda zaidi ya mikoa 20.
    “Kwenda mkoa mmoja natumia siku mbili ama tatu kufika na kupata wadhamini. Gharama ni nyingi sana, lakini kwa kuwa nimeshaamua kuwatumikia Watanzania nitakwenda,”alisema.
    Alisema Watanzania wamekuwa wakimtia matumaini katika safari yake hiyo na kuwaomba wamuombee ili aweze kuifanikisha kwa mafanikio.
    “Naomba Watanzania wenzangu mniombee katika safari hii. Nitawavusha kuwapeleka kwenye nchi ya ahadi,” alisema Bilohe aliyejiunga na chama hicho mwaka 2003.
    Alisema kuwa atazirudisha fomu hizo Juni 30 au Julai Mosi kulingana na ratiba yake ya kukusanya wadhamini.
    Jumla ya makada 39 wamejitokeza kuwania nafasi hiyo na Bilohe ndiye mgombea pekee aliye na elimu ndogo ya darasa la saba, tofauti na sheria ya nchi inayotaka mgombea wa nafasi hiyo ya juu kisiasa awe na shahada.
    Bilohe ni mmoja wa makada wachache waliojitokeza kuomba ridhaa ya CCM ambao hawajawahi kushika madaraka makubwa serikalini au ya kisiasa.
    Katika kinyang’anyiro hicho kuna mawaziri wakuu watatu, mawaziri 12 wa sasa, Jaji Mkuu mstaafu, maofisa wa juu wa Idara ya Usalama wa Taifa, maofisa waandamizi wa Serikali ambao wamestaafu na 
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: Mkulima atumia mabasi kusaka wadhamini Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top