Mara nyingi nimesikia ndani ya vikao vya Bunge kuhusu ishu ya jinsi kuwahamisha watu wanaoishi pembeni ya Viwanja vya ndege ili Viwanja vitanuliwe.. kuna waliofuata Viwanja na kuanzisha makazi yao, ishu ni Kiwanja kiondoke kwenda mbali au watu waondolewe viwanja vitanuliwe?
Oslo-Torp Airport.. Huu uwanja uko umbali wa Kilometa 117 kutoka Oslo ambapo ni Mji Mkuu wa Norway. Ukitaka kufika Town inabidi utumie taxi au usafiri wa treni.
Munich West Airport. Ukisikia jina la huu Uwanja unaweza kuhisi kwamba uko ndani ya Mji Mkuu wa Ujerumani, Munich. Lakini ukweli ni kwamba Uwanja huu wa ndege uko Memmingen. Na bado Umbali wa kutoka Uwanjani mpaka kwenye Mji ni Kilometa 112.
Frankfurt (Hahn). Uwanja huu wa Ndege uko umbali wa kama kilometa 109 kutoka Mji wa Frankfurt, Ujerumani.
Ndani ya Ujerumani mtu wangu, hapa ni Dusseldorf Airport.. Kutoka hapa mpaka kufika katikati ya Jiji la Dusseldorf ni Kilometa 49 pia.