China imeingia ingia kwenye headlines baada ya ulaji wa nyama ya mbwa kuongezeka nchini humo. Hapo awali ulaji wa nyama hio ulikatazwa nchini China baada ya kuonekana kua ulaji wa nyama hio ni kinyume na utaratibu wa kibinadamu kwa sababu mbwa walionekana kua viumbe venye thamani kubwa kwenye maisha ya bindamu, kwenye ulinzi na hata uwindaji pia.
Hali iko tofauti kwa karne hii ya 21 nchini China kwani ulaji wa nyama ya mbwa umeongezeka licha ya kitendo hicho kukatazwa kwa zaidi ya miaka hamsini
iliopita. Kuongezeka kwa vitendo hivi kumesababisha mjadala mkubwa
nchini humo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya watu ambao wanapinga
kitendo hicho huku wakidai ulaji wa nyama ya hio ni ukatili dhidi ya
wanyama hao, na ni kitendo kinacho dumisha dhana potofu za ulaji wa
nyama ya mbwa.
Kutokana na historia ya China, Guangzhou
ni mji unaofahamika kwa watu wanao ongoza kwa ulaji wa nyama ya mbwa,
lakini hivi karibuni mgahawa maarufu wa nyama ya mbwa ulilazimika
kufunga biashara baada ya miaka 51 ya utengenezaji wa nyama hio jijini hapo baada ya vita dhidi ya watetezi wa haki za wanyama wa kufugwa (Domestic Pets). Licha ya hivyo, uchinchaji wa mbwa kwa ajili ya uuzaji wa nyama ulikua maarfu sana jijini Beijing lakini kitendo hichi kilifika mwisho miaka 10 iliopita kutokana na Sheria mpya iliokataza kitendo hicho.
Bado kuna miji ambayo vitendo vya ulaji
wa nyama ya mbwa vinaendelea kwa kiasi kikubwa, ila maandamano ya
kukomesha tabia hii yameshaanza kwa baadhi ya miji nchini humo, wakiwa
na dhamira ya kukomesha kitendo hicho.