Maombi yamefanyika katika taifa la Marekani, baada ya kuuwawa kwa watu tisa katika kanisa la kihistoria la Wamarekani wenye asili ya Afrika la Charleston, huko South Carolina.
Mtuhumiwa wa mauaji hayo ya chuki za kibaguzi Dylann Roof, mwenye umri wa miak 21, alikamatwa katika kizuizi cha polisi wa barabarani huko Shelby, North Carolina.
Katika tukio hilo wanawake sita wanaume watatu akiwemi mchungaji wa kanisa hilo walikufa, na tayari uchunguzi wa uhalifu utokanao na chuki umeanza.
Imeelezwa kuwa kijana huyo mweupe alipatiwa silaha aliyotumia kwa mauaji kama zawadi ya kuzaliwa.