WABUNGE watatu kutoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wameishambulia Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba, imechoka kufikiria wananchi.Anaripoti Dany Tibason … (endelea).
Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila na Mbunge wa Kasulu Mjini, Mosses Machali wote wa NCCR-Mageuzi) pia Mbunge wa Maswa, Sylvester Kasulumbayi (Chadema) wamesema, CCM imeshindwa kubuni vyanzo vya mapato ili kuiondoa nchi hapa ilipo.
Kasulumbayi amesema kuwa, mbali na kushindwa kubuni vyanzo vipya vya mapato, serikali imekuwa ikiwatapeli wazee juu ya ongezeko la pensheni.
Mbunge huyu ametoa kauli hiyo bungeni leo alipokuwa akichangia katika hoyuba ya bajeti ya Wizra ya Fedha iliyowasilishwa wiki iliyopita na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.
Akichangia amesema, ni maajabu serikali kushindwa kuwa wabunifu wa kutafuta vyanzo vipya vya mapato na badala yake imekuwa ikitafuta vyamzo ambavyo vinagusa moja kwa moja maisha ya mtanzania wa kipato cha chini.
Amesema, imekuwa ni kawaida ya serikali kutafuta vyanzo vya mapato kwa bidhaa zile zile ambazo ni sigara na pombe na kuacha vyanzo vingine ambavyo vinaweza kuliongezea taifa pato kubwa.
“Hapa tukisema serikali imechoka tunaonekana kama tunawatukana lakini inakuwaje serikali inashindwa hata kutafuta vyanzo vya mapato kupitia katika mifugo.
“Tanzania ni nchi ya tatu katika bara la Afrika kwa kuwa na mifugo mingi lakini kutokana na serikali kutokuwa na ubunifu imeshindwa kutambua kama mifugo hiyo inaweza kuwaingizia pato,” amesema Kasulumbayi na kuongeza;
Serikali imechangia kwa kiasi kikubwa Watanzania kuwa masikini na sasa wanaendelea kuwafanya kuwa masikini kwa kuweka kuongeza tozo ya mafuta ya dizel, petrol na mafuta ya taa.
Amesema, anasikitishwa na serikali kuiona mifugo kama sehemu ya uharibifu wa mazingira badala ya kutafuta njia bora ambayo inaweza kusababisha ikaongeza pato la taifa.
Akizungumzia kuhusu ongezeko la pensheni kwa wazee amesema, serikali bado inawalaghai wazee kwa kudai kuwa itawaongezea pensheni kwa kuwapatia sh.85,000.
“Serikali inawapiga change la macho wazee haiwezekani mpaka leo serikali inadai haina idadi kamili ya wazee wakati sensa ya watu na makazi inawatambua wazee ni wangapo, akina mama, vijana, watoto na wanawake.
“Imekuwa kawaida ya CCM kuwa na vipaumbele ambavyo vinaonekana kuwa vizuri kwa mipango lakini utekelezaji ni wa hovyo na hautekelezeki na ndiyo maana tunasema serikali imechoka,” amesema Kasulumbayi.
Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) amesema umasikini ambao unawakumba Watanzania umesababishwa na Serikali ya CCM hususan ya awamu ya nne.
Akichangia katika bajeti kuu ya serikali Kafulila amesema, sababisho kubwa la umasikini unatokana na uzembe wa serikali kushindwa kutafuta vyanzo vipya vya mapato.
Amesema, ni aibu kwa wanafunzi kuendelea kukalia mawe wakati kuna uwezekano mkubwa wa serikali kutumia mistu ambayo inaweza kutumika kuchana mbao na kutengeneza madawati.
“Yaani tukisema serikali imechota siyo kuwa tunawatania bali tunasema kweli nyinyi viongozi mmechoka na hapa ndiyo maana tunajadili Bajeti muhumu ya serikali lakini mawaziri hawapo, wanakimbia na mbio za urais huu ni uzembe wa hali ya juu,”amesema.
Mbunge wa Kasulu Mjini, Mosses Machali (NCCR-Mageuzi) amesema, kitendo cha wabunge kushindwa kukaa bungeni na kujadili bajeti muhimu ni dalili kuwa wabunge wengi hawajiamini.
Amesema, kila mbunge atapimwa na matendo ambayo aliyafanya jimboni na kama alifanya vyema ni wazi kuwa wapiga kura wake watamchagua.
Akichangia hoja Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby (CCM)alikubaliana na ongezeko la tozo ya mafuta huku akisema fedha za tozo hizo zifanye kazi ambayo imekusudiwa.
Amesema imekuwa tabia ya serikali kutofanya kazi ambayo imekusudiwa na badala yake imekuwa ikitoa fedha kinyume na mapitisho au maazimio ya bunge.
Mbali na hilo amesema, anasikitishwa na serikali kushindwa kuwalipa wakulima fedha ambazo wanadai kutokana na kuwahuzia mahidi.
CREDIT : http://mwanahalisionline.com/