https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    CHADEMA wapuuza taarifa ya Jeshi la Polisi kuruhusu mikutano ya ndani ya vyama vya siasa. Wamesema kisheria polisi hawana mamlaka ya kuzuia au kuruhusu. -






    Tumeipuuza kauli ya jana ya Jeshi la Polisi, kama tulivyolipuuza tamko lao la awali walilolitoa Septemba 24, mwaka huu. Walipopiga marufuku mikutano ya ndani.

    Tunalipuuza tamko lao la jana kwasababu hata walipopiga marufuku sisi tulikuwa tukiendelea na mikutano ya ndani kama kawaida, Hatukukubaliana nao hapo awali kwahiyo hatuwezi kujitokeza kuwapongeza. Tunaendelea kuwapuuza.

    Sisi kama Chama, hatuwezi kuruhusu ufunguo wa demokrasia uwe mikononi mwa Jeshi la Polisi. 
    Hali hii tunaikataa na tutaendelea kuikemea kwani kama chama hatuwezi kuruhusu kuongozwa kwa matamko yasiyo na mashiko kisheria.

    Pili, tunazo taarifa kuwa Chama Cha Mapinduzi kimepanga kuanza vikao vyake vya ndani.

    Nadhani mliona hata Rais Magufuli alipotembelea Uhuru, alipotaka kufanya baadhi ya maamuzi, Katibu Mkuu Kinana alinukuliwa akisema maamuzi hayo yatafanywa na vikao vya chama.

    Kwahiyo CCM wanahitaji kufanya vikao ambavyo ni haki yao kabisa kisheria.

    Lakini tunazo taarifa kuwa, Jeshi la Polisi limeruhusu mikutano CCM itakapoanza vikao vyake vya ndani isionekane kuwa wanakiuka maagizo ya Jeshi la Polisi.

    Walifanya hivyo kipindi cha nyuma, wakatoa tamko kuwa wanafungia vikao vyote na mikutano ya vyama lakini ulipokaribia mkutano mkuu wa CCM wakaruhusu vikao vya ndani.

    Na hata sasa msishangae baada ya CCM kumaliza vikao vyake vya ndani wiki mbili zijazo, Jeshi la Polisi wakajitokeza tena na kusema hali ya usalama imekuwa tete kwahiyo wanazuia tena mikutano ya ndani ya vyama vya siasa.

    Tunaonya na kulaani tabia hii ya Jeshi la Polisi kutumika kisiasa
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CHADEMA wapuuza taarifa ya Jeshi la Polisi kuruhusu mikutano ya ndani ya vyama vya siasa. Wamesema kisheria polisi hawana mamlaka ya kuzuia au kuruhusu. - Rating: 5 Reviewed By: news
    Scroll to Top