Ijumaa
ya Septemba, 23 aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania na Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Taifa ya CHADEMA, Edward Lowassa amewasili mkoani
Kagera kwa ajili ya kuwajulia hali waathirika wa tetemeko la ardhi
ambalo lilitokea Septemba, 10 mwaka huu.
Baada
ya kuona hali ilivyo sasa kwa baadhi ya wakazi wa mkoa huo kupoteza
ndugu zao, nyumba na mali zao kuharibika, Lowassa ametumia ukurasa wake
wa Twitter kufikisha ujumbe kwa jamii ya watanzania sehemu yoyote walipo
duniani kote.
Ujumbe
wa kwanza Lowassa aliandika “Poleni ndugu zangu Wa Kagera na
mlioathirika na tetemeko, Tupeane nguvu ili tuvuke katika kipindi hiki
kigumu pamoja”
Na
ujumbe wa pili Lowassa aliandika “Nawasihi watanzania wenzangu
tuendelee kujitolea kuwasaidia wahanga kama ilivyo desturi ya umoja wa
kitaifa tulionao”
0 comments:
Post a Comment