Picha
ya Omran Daqdees mwenye miaka mitano ambayo alionekana akiwa na vumbi
na damu baada ya nyumba yao huko Aleppo Syria kuharibiwa katika mlipuko,
picha hiyo iliwashtua wengi duniani mwezi uliopita ikiwa
ni pamoja na mvulana aitwaye Alex, ambaye anaishi Scarsdale, New York.
Alex imembidi amwandikie barua President Obama ikiwa na mstari unaosema
‘atakuwa mwanafamilia mwenzetu na atakuwa kaka yetu’
Baada ya kupokea barua hiyo Rais Obama ameishare video kwenye ukurasa wake wa facebook yenye barua hiyo na kuandika hivi…………
>>>Alex
ni mtoto mwenye miaka sita. Anaishi Scarsdale, New York Marekani, mwezi
uliopita kama watu wengine duniani aliguswa na taarifa za picha za
mtoto Omran Daqneesh, mwenye umri wa miaka mitano huko Aleppo Syria,
aliyekuwa amekaa kwenye gari la wagonjwa (Ambulance) akiwa na taharuki
huku akijaribu kujifuta damu mikononi mwake.
>>>Hivyo
Alex alikaa chini na kuniandikia barua, wiki hii katika mkutano wa
Umoja wa mataifa uliokuwa ukijadili masuala ya wakimbizi,
niliishirikisha dunia maneno mazito ya Alex.
>>>Alex
aliniambia alitaka Omran aende kuishi naye pamoja na familia yake,
alitamani atumie naye baisikeli yake, pia amfundishe jinsi ya
kuiendesha. Akasema dada yake atakuwa akimkusanyia vipepeo, na watakuwa
wakicheza wote pamoja, akaandika “Tutamfanya familia na atakua kaka
yetu.
>>>Hayo
ni maneno ya mtoto wa miaka sita ambaye bado hajajifunza kutuhumu au
kuwa na wasiwasi na woga kwa watu wengine kulingana na walipotoka,
wanavyoonekana ama jinsi wanavyo abudu.
>>>Inabidi
nasi tuwe kama Alex, fikiria dunia ingekuwaje kama tungekua kama yeye.
Tafakari tugepunguza maumivu kiasi gani na tungeokoa maisha ya watu
wangapi. Msikilize Alex, soma barua yake, na ninafikiri utanielewa kwanini niliushirikisha ujumbe huu kwa dunia.
0 comments:
Post a Comment