Headlines zina stori nyingi za wazamiaji toka Nchi za Afrika Kaskazini kwenda nchi za Ulaya, na njia kubwa wanayoitumia ni usafiri wa kwenye maji, unajua kwamba kuna uzamiaji wa kwenye ndege pia?
Stori za wazamiaji wa kwenye ndege ziko chache labda kwa sababu ya Sheria na taratibu za kupanda ndege zilivyo ngumu, jamaa wawili wameingia kwenye headlines baada ya kuzamia kwenye ndege ya Shirika la British Airways toka Johannesburg, South Afrika mpaka Heathrow, Uingereza.
Mwili wa mmoja wao umekutwa juu ya jengo moja maeneo ya Richmond, jirani na Uwanja huo wa ndege, mwingine amekutwa kwenye ndege hiyo na hali yake sio nzuri.. kapelekwa Hospitali kwa ajili ya matibabu.
Polisi hawajathibitisha tukio la mwili wa mtu aliyekutwa juu ya jengo na aliyekutwa kwenye ndege kama wote walikuwa wazamiaji toka South Africa… Mtu mmoja ambae amekutwa hai na kukimbizwa Hospitali alikuwa amejificha kwenye sehemu ya tyre za ndege.
Nina kipisi cha Video ya hiyo stori hapa.