KIUNGO chipukizi wa Ghana, Joseph Tetteh Zutah na mshambuliaji wa Zimbabwe, Donald Ngoma kwa pamoja wametua leo nchini kwa ajili ya kuja kujiunga na Yanga SC.
Zutah aliyezaliwa Agosti 22, mwaka 1994 anatokea klabu ya Medeama ya kwao, wakati Ngoma anatokea FC Platinum ya kwao pia na wote watafika asubuhi.
Yanga SC imekwishafanya mazungumzo ya awali na wachezaji hao na wanatarajiwa kuja kusaini mikataba.
Yanga SC iliitoa Platinum katika hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu, lakini kocha Mholanzi Hans van der Pluijm akavutiwa mno na Ngoma, aliyecheza mechi moja tu ya Zimbabwe baada ya kukosa mechi ya Dar es Salaam kwa sababu alikuwa majeruhi.
Na Pluijm ambaye amewahi kufundisha Ghana, ndiye aliyempendekeza Zutah ambaye uongozi wa Yanga SC haujawahi kumuona kabisa, lakini vyanzo vinasema huyo ni mchezaji mzuri anayeweza kucheza pia kama beki wa kulia.