Watu wenye silaha wanaoshukiwa kuwa ni wapiganaji wa kundi lenye kufuata itikadi kali za Kiislam la al-Shabaab, jana usiku wamemuua Chifu mmoja nchini Kenya katika mpaka wa kaskazini mashariki mwa mji wa Wajir.
Chifu huyo Mohammed Barre wa eneo la Erib huko Wajir, alipigwa risasi na kufa na watu waliokuwa na silaha waliokuwa wakimfuatilia wakati akitoka msikitini, ambako alienda kuswali swala ya mwisho ya usiku.
Kamanda wa polisi wa kaunti ya Wajiri Samuel Mukindia amethibitisha kuuwawa kwa chifu huyo aliyemuelezea kuwa alikuwa mtumishi wa serikali muadilifu, ambapo amesema alipigwa risasi umbali wa mita 500 kutoka msikitini.