Waziri
William Vangimembe Lukuvi akisisitiza jambo baada ya Watendaji wa sekta
ya ardhi ya Mkoa wa Lindi kushindwa kumudu maswali mbalimbali
aliyowauliza na kuwataka watendaji hao kujipima kama bado wanastahili
kuendelea kuwatumikia wananchi kwa nafasi zao wanazotumimkia.
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi Mh. Mwantumu Mahiza akimuomba Mheshimiwa William
Lukuvi kuwaondoa watendaji wabovu wa sekta ya ardhi Mkoani Lindi akisema
kuwa wapo watanzania wengi wenye uwezo wa kufanya kazi zao. Alisema
kuwa hayuko tayari kuyumbisha kiti chake alichoaminiwa na Rais kwa
kuwalea watendaji wazembe.
Sehemu
ya umati wa wananchi waliofika eneo la Mitwero kuwasilisha kero zao kwa
Waziri William Lukuvi. Malalamiko mengi ya wananchi yanatokana na
kutokushirikishwa katika uthamini wa ardhi na mali yao hali ambayo
imewafanya kupunjwa malipo ya fidia. Waziri Lukuvi ameagiza wanaothamini
mali ya wananchi kote nchini kufanya kazi hiyo kwa uaminifu na
kuwashirikisha wananchi hao katika hatua zote ili kuondoa malalamiko na
kutenda haki.
Waziri
Lukuvi akimhoji Mpima ardhi wa MANISPAA YA Lindi Bw. Mpoki baada ya
kulalamikiwa na wananchi wengi kuwa anatabia ya kuomba rushwa ili kuwapa
huduma wananchi. Waziri Lukuvi ameapa kutomsamehe Afisa yeyote wa sekta
ya Ardhi atakayetajwa na wananchi na kubainika kula rushwa na kwamba
uchambuzi wa malalamiko ya wananchi ukikamilika ataanza kuchukua hatua
za kinidhamu kwa watendaji wabovu na wala rushwa.
Mwananchi
aliyebahatika kutoa dukuduku zake kwa Waziri Lukuvi akimuonyesha Afisa
anayelalamikiwa kwa rushwa katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero
za wananchi eneo la Mitwero lililopo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi.
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi Mh. Mwantumu Mahiza atiktoa taarifa ya migogoro ya
Ardhi ya Mkoa wa Lindi kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi alipowasili Ofisini kwake.
Sehemu
ya Watendaji wa Mkoa wa Lindi wakiwemo Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi
wa Halmashauri za Wilaya wakimsikiliza Waziri Lukuvi(hayupo pichani)
alipozungumza nao katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kusisitiza
uadilifu katika sekta ya ardhi ili kuhudumia wananchi kwa haki na
kuondoa kero za ardhi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi
akiongea jambo na Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya
alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa LindI tayari kuanza kikao
cha Watendaji wote wa Mkoa huo.
Mheshimiwa
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akishangazwa na uamuzi
wa Manispaa ya Lindi wa kupimiwa ardhi na UTT kwa gharama kubwa jambo
ambalo wangelifanya wao ili kujenga uzoefu, kupata faida kubwa na
kupunguza gharama ya kupima na hatimaye kuuza viwanja hivyo kwa
wananchi. Ameagiza kupitiwa upya makubaliano waliyofanya na UTT ili
kupata fedha za kuwaongeza fidia wananchi wanaolalamikia kupunjwa fidia
eneo la Mitwero, nje kidogo ya Manispaa ya Lindi.
Wananchi
kadhaa wakimpongeza Waziri Lukuvi kwa kuweza kutatua migogoro yao ya
ardhi iliyodumu kwa miongo miwili na zaidi alipomaliza mkutano wa
kuwasikiliza na kuagiza mambo mbalimbali ya kuondoa kero za wananchi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi
amemaliza ziara ya siku mbili Mkoani Lind ambapo alikagua shughuli za
Shirika la Nyumba la Taifa na kusikiliza migogoro ya ardhi inayowakabili
wananchi wa Lindi eneo la Mitwero na kuitatua.
Katika
ziara hiyo, Waziri Lukuvi amewaonya na kuwaagiza Maafisa ardhi, wapima
na maafisa mipango miji kuacha mara moja kujinufaisha kwa kuwadhulumu
wananchi haki zao za ardhi.
Aidha
ameutaka Mkoa wa Lindi kuharakisha upimaji wa ardhi ya wananchi na
utoaji wa hati ili kuwawezesha wananchi kumiliki ardhi na kupunguza
migogoro ya ardhi.