Staa wa filamu za Kibongo,Wema Sepetu ametajwa kuwa ndiye aliyechangia kwa kikubwa ushindi wa tuzo tano za Killi za msanii wa Bongo Fleva,Ali Kiba kutokana na kumpigia debe mara nyingi kupitia akaunti yake ya Instagram.
Akifunguka kupitia 255 ya XXL,Wema alisema kuwa Ali Kiba alimuomba ampigie debe kwenye akaunti yake ya Instagram,kwani hata msanii huyo aliwahi kumpigia debe alipowania tuzo za Watu ndiyo maana alifanya hivyo.