Klabu ya Yanga imethibitisha kuvunja mkataba na mshambuliaji wake Said Bahanuzi kutokana na kushuka kwa kiwango chake kwa miaka mitatu mfululizo.
Katibu mkuu wa Yanga Dkt. Jonas Tiboroha amesema kwamba, Yanga haijaridhishwa na maendeleo ya Bahanuzi aliyekuwa anacheza kwa mkopo katika klabu ya Polisi Morogoro kwa msimu uliopita, hivyo anatolewa kama ilivyotokea kwa Jeryson Tegete na Omega Seme.
“Bahanuzi ni moja ya wachezaji tuliovunja nao mikataba kwasababu klabu haijaridhishwa na maendeleo yake kama ilivyo kwa wachezaji wenzake akina Omega, Thabit, Jerry Tegete”, zmesema Tiboroha.
“Mikataba ya Yanga inaangalia kiwango cha mchezaji, kama mchezaji hana kiwango cha kuendelea kucheza Yanga anaachwa, tunavyo vipengele vinavyoeleza wazi”, aliongeza Toboroha.