Azam FC ambao ni wawakilishi
pekee wa Tanzania kwenye michuano ya Kagame Cup wafanikiwa kutinga
fainali ya mashindano hayo baada ya kuilaza KCCA ya Uanda kwa goli 1-0
kwenye mchezo wa nsu fainali uliomalizika jioni ya leo kwenye dimba la
Taifa.
Goli pekee la Azam limefungwa na
Shah Farid Mussa dakika ya 76 kipindi cha pili na kuihakikishia Azam
kucheza fainali ya Kagame kwa mwaka 2015.
Kipindi cha kwanza kilimalizika
huku timu hizo zikienda mapumziko zikiwa sare ya bila kufungana (1-1)
lakini timu zote zikiwa zimepoteza nafasi za kufunga kwenye kipindi cha
kwanza. Jonh Bocco na Kipre Tchetche kila mmoja alikosa nafasi ya
kufunga kwa wakati wake baada ya Azam kufanya mashambulizi mawili ambayo
yalikuwa ni makali.
Sserunkuma Isaac wa KCCA nae
alikosa goli baada ya kipa wa Azsam FC Aishi Manula Salum kuokoa mpira
uliokuwa unaelekea golini kabla hajapumzishwa kumpisha Kondo Shaban
mabadiliko ambayo yalifanywa ndani ya kipindi cha kwanza
Kipindi cha pili Azam walianza
kwa kufanya mabadiliko ambapo walimpumzisha Mudathir Yahya na nafasi
yake ikachukuliwa na Ame Ally ‘Zungu’ na baadae akaingia Shomari Kapombe
huku Erasto Nyoni akienda kwenye benchi na Kipre Tchetche akatolewa
kumpisha
Mwanzoni mwa kipindi cha pili,
KCCA ilifanya mashambulizi kadhaa golini kwa Azam lakini uimara wa ukuta
wa Azam uliweza kuhimili kashikashi hizo.Huku KCCA wakionekana kutawala
mchezo katika eneo la katikati na kucheza mipira mirefu hali iliyowapa
ugumu Azam.
Kadiri muda ulivyokuwa ukiyoyoma
Azam walionekana kuelemewa kwani Manula alifanya kazi ya ziada kuokoa
kombora la Ochaya Joseph alilopiga akiwa nje ya eneo la mita 18.
Baada ya Azam kupata goli, KCCA
walifanya mabadiliko kwa kumpumzisha Habibu Kavuma na kumuingiza Birungi
Michael lakini bado mabadiliko hayo hayakuzaa matunda kwa upande wao
kwani hadi filimbi ya mwisho ya mwamuzi Souleiman Ahmed kutoka Djibouti
Azam waliweza kutoka uwanjani wakiwa mbele kwa goli 1-0 na kutinga
fainali ya Kagame kwa mara ya pili katika hisoria yao
Azam sasa watacheza na Gor Mahia
ya Kenya kwenye mchezo wa fainali unaotarajiwwa kuchezwa siku ya
Jumapili. Gor Mahia walifuzu kucheza fainali baada ya kuifunga Khartoum
ya Sudan kwa goli 3-1 kwenye mchezo uliotangulia mchana wa leo.
0 comments:
Post a Comment