https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    BAADA YA KUNUSURIKA KWENYE TSUNAMI NA KUSAIDIWA NA CRISTIANO RONALDO…DOGO ASAINIWA NA SPORTING LISBON

    t3
    Wataalam wa mambo wanasema ndoto yako ukiisimamia vizuri na kuifanyia kazi lazima itatimia siku moja. Story ya Martunis ambae alivyoka na miaka 8 alizolewa na maji na kusukumwa hadi beach na kujikuta amekaa kwenye dimbwi la maji karibu na bahari. Alikaa hapo kwa muda wa siku 18 akila vyakula vilivyosombwa na maji kuletwa hapo alipo baada ya Tsunami kutokea.
    Alikutwa hapo na mwandishi wa habari wa Sky News akiwa amevaa jezi namba 10 ya mchezaji wa Portugal Rui Costa ambayo alikua amevaa wakati anasombwa na maji. Alivyoulizwa kuhusu jinsi alivyonusurika kifo Martunis alisema kwamba “Nilikua siogopi kwa wakati ule kwasababu bado nilikua nataka kuendelea kuishi na kuwaona ndugu zangu na pia kuwa mcheza mpira”
    t1
    Story yake iligusa nyoyo za watu wengi akiwemo mchezaji wa Portugal Cristiano Ronaldo na akamlipia ujenzi mpya wa nyumba yao ambayo iliharibiwa na Tsunami. Martunis ameshakutana na Cristiano Ronaldo mara nyingi na hivi karibuni alikutana nae mwaka 2013. Mwaka 2005 Martunis alikutana na kikosi cha Portugal akiwemo shujaa wake CR7 na akasema siku moja angependa kuchezea timu ya taifa ya Portugal.
    t2
    Habari nzuri kwa sasa ni kwamba Martunis atacheza timu ya under 19 akiwa na club ya Sporting Lisbon ambapo Cristiano Ronaldo alipitia. Lisbon imesajili mchezaji huyo ambae toka kitambo alikua na ndoto za kucheza soka.
    t4
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BAADA YA KUNUSURIKA KWENYE TSUNAMI NA KUSAIDIWA NA CRISTIANO RONALDO…DOGO ASAINIWA NA SPORTING LISBON Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top