Inasemekana kuwa, Gervinho alitoa sharti la kupewa helicopter pamoja na sehemu ya eneo la beach (binfsi) ili akubali kujiunga na klabu ya Al-Jazira.
Lakini mshambuliaji huyo amesema “nimesoma kuhusu helicopter pamoja na beach binafsi. Sijui habari hizo zinatoka wapi, kamwe sijaomba vitu kama hivyo”.
Ninaposaini mkataba huwa sitazami vitu kama hivyo, kilakitu kilichosemwa kuhusu hilo ni uongo”.
Al-Jazira wameongeza: “tunathibitisha kusitisha mazungumzo na Gervinho lakini hii ilikuwa ni kwa ajili ya mahitaji ya benchi la ufundi na sio matakwa ya mchezaji tofauti na ilivyoripotiwa na baadhi ya habari za mtandaoni”
Klabu yetu imefikia makubaliano na Roma kwa ajili ya huduma ya mchezaji huyo kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 13.
Gervinho alijiunga na Roma akitokea Arsenal mwaka 2013 na msimu uliopita alifunga jumla ya magoli 24 kwenye ligi ya Siria A.


0 comments:
Post a Comment